Wiki chache zilizopita kulikua na kurushiana kwa maneno kati ya madirector wa Bongo Adam Juma wa Next level na Nisha wa Nisha Entertainment,,,Millardayo.com imepiga xclusive na Director John Kallage wa Kalla pics ambaye amesema
‘Aaah well hizo mi mi nimefatilia kwa sehemu moja au nyingine lakini kiukweli sijui yani nisemaje lakini mi naona kwanza hayo mambo hayanihusu kwa sababu hayo mambo ni parsonal ni mtu mmoja na mtu mwingine ndo wamegombana hayanihusu,lakini kwa ufatiliaji nilivyoona naona kwenye hilo tatizo kuna mmoja hana adabu’.
‘Ukweli kama mioyoni mwao wako real kwamba wanabishana wana fanya malumbano hayo kwa kupeana challenge za kikazi hilo sidhani hata kama wewe utakataa kwamba halitoendeleza game lakini kama wanafanya mambo ya mitaani ya hivi na hivi kama mioyoni mwao wana bifu tofauti hiyo haiwezi saidia chochote’
‘Mashabiki wajaribu kuangalia tu kazi nyingi tunazozifanya kwa sababu kazi ni nyingi na mimi mwenyewe naendelea kufanya japo nguvu kubwa nimeiweka kwenye filamu kwa sababu huko ndipo nilipokuwa nimeanzia’.