Matukio yanayokiandama chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] yamezidi kuchukua nafasi ambapo mkoani Arusha watu wasiojulikana wameshutumiwa kuchoma moto ofisi za chama hicho Jumanne tar 03 Dec 2013 asubuhi na kusababisha uharibifu mdogo.
katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Mchungaji Amani Golugwa amesema ‘Mpaka hivi sasa tunavyoongea eneo la ofisi ndani ya ofisi kabisa eneo la bafu na choo limeungua na upande wa juu wa bati umeungua na kikubwa zaidi walitaka kuingia chumba cha computer room ambacho tunahifadhi data kwa wanachama wetu kwa kanda nzima ya kaskazini majimbo 33 sasa hivi’
‘Sasa baada ya kushindwa hiyo ndo wakatengeneza shoti ya umeme pakashika moto, tunamshukuru Mungu tu kwamba huu moto haukuendelea sana kwa hiyo athari haipo kwenye nyaraka zozote wala kwenye machine zilizopo hapa ofisini’ – Golugwa
‘Ni mapema mno kulizungumzia hasa kuliunganisha na kinachoendelea sasa hivi kwenye chama lakini hisia zetu za ndani zinatupeleka mahali fulani ambapo bado ni mapema kulielezea lakini ni tukio ambalo limetufedhehesha na kutushangaza hasa lengo lilikua ni kuiunguza ofisi yote, bila kujali majirani waliopo hapa na vitu vya thamani hasa hizo data zilizopo kwenye mashine zetu japo hua tunafanya back up ya kila siku lakini ni kitu ambacho kimetushtua sana’.
‘Ukweli yanayoendelea sasa hivi watu wengine wanaweza wakatafsiri ni migogoro ndani ya chama lakini ukweli ni kwamba chama kinajisafisha…. chama kinatumbua majipu nitumie kauli hii kama mtu mwilini una majipu hamsini huwezi ukasema utumbue majipu mawili au matatu uyaache useme umepona utayatumbua yote kwa hivyo kinachoendelea sasa hivi ni bundi ametua Chadema, ni bundi anafukuzwa kwa hivyo tuna mambo mengi yanayokuja na kwa uzoefu wangu wa kisiasa ninaelewa kwamba zoezi tunalolifanya sasa hivi la kushughulikia wahaini, wasaliti linaweza kuwa la maumivu kwa wale ambao walikua na nia mbaya na malengo mabaya ndani ya chama kwa sababu mpango wao umeshindwa’