Quantcast
Channel: Millard Ayo
Viewing all articles
Browse latest Browse all 31461

Hivi ndivyo wananchi wa Kigoma walivyompokea Zitto Kabwe

$
0
0

DSC_0333Leo Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe  amehutubia wananchi wake wa Kigoma kwa mara ya kwanza mkoani hapa tangu avuliwe nyadhifa zake zote ndani ya chama chake cha Chadema.

zito13Zitto alifika kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma saa tatu asubuhi na kufuatiwa na maandamano yaliyoanzia ofisi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwenda kusaini kisha yakaendelea mpaka  kijijini kwao Mwandiga mchana wa leo na kufuatiwa na mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa eneo hilo wakiwa wamebeba Mabango mbalimbali.

zito12Miongoni mwa  mabango hayo yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao kuna yaliyosomeka Zitto Kama Nyerere, Zitto kama Mandela Kasoro Jela, Zitto rais wetu 2015,waha siyo nguruwe,karibu mwamba wa siasa,Zitto kama Nyerere,Mandela wa Tanzania karibu Kigoma na mengine mengi.

zito10Akihutubia mamia ya wananchi waliokusanyika kwenye uwanja Mwandiga Zitto alisema mwaka  2006  wananchi wa Kigoma mlifanya tena maandamano na mapokezi kama haya  mlipokuwa mnanipokea baada ya kusimamishwa ubunge na wana CCM nilipokuwa natetea maslahi ya wananchi, safari hii hali hii imetokea kutokana na changamoto nilizonazo kwenye chama changu.

DSC_0230“Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali anasema mimi nimekataa kuhojiwa na kamati yake wakati ukweli ni kuwa nilikutana nao kama mara nne,hadi kuna kipindi walikuja kunihoji kipindi nko kwenye kambi ya mafunzo ya Jkt najua wanafanya hivi kwa sababu kwa sasa hivi suala la fedha zilizofichwa nje ya nchi zimeshikwa na watu hatari,’Zitto anategemea kuendelea na ziara yake kesho kwa wilaya ya Kasulu.

zito18

zito17

DSC_0230

DSC_0333

v

zito8

zito14

 

Use Facebook to Comment on this Post


Viewing all articles
Browse latest Browse all 31461

Trending Articles