Michuano mikubwa kwa ngazi ya vilabu duniani UEFA Cahmpions League ilianza rasmi hapo jana ambapo viwanja nane barani humo vilishuhudia timu 16 zikivaana .
Kocha wa Manchester United David Moyes akiwa anaiongoza Manchester United kwenye ligi ya mabingwa kwa mara yake ya kwanza aliweza kupata ushindi wa 4-1 dhidi ya Bayer Leverkusen .
Mshambuliaji Wayne Rooney alikuwa nyota wa mchezo akifunga mabao mawili na kutengeneza bao lingine lililofungwa na Antonio Valencia huku Robin Van Persie naye akifunga bao moja . Mabao mawili ya Bayer Leverkusen yalifungwa na Simon Rolfes na Beki Omer Toprek .
Ushindi mkubwa kuliko yote kwa usiku wa jana (Jumanne) ulikuwa nchini Uturuki ambako Cristiano Ronaldo aliwaongoza Real Madrid kupata ushindi wa 6-1 mbele ya wenyeji wao Galatasaray . Ronaldo alifunga mabao matatu peke yake huku Isco , Karim Benzema wakifunga mabao mengine . Umut Bulut alifunga bao pekee la Galatasaray .
Paris St Germain wanaocheza michuano hii kwa msimu wao wa pili mfululizo waliwafunga Olympiakos 4-1 katika mchezo uliopigwa nchini Ugiriki.
Mabingwa watetezi wa michuano hii Bayern Munich waliwafunga CSKA Moscow 3-0 . Mabao ya Bayern yalifungwa na David Alaba , Arjen Robben na Mario Mandzukic .
Man City wakiwa ugenini nchini Poland walishinda mchezo wao dhidi ya Viktoria Plzen kwa 3-0 . Yaya Toure,Edin Dzeko na Sergio Aguero ndio walifunga mabao ya City kwenye mchezo huo .
Katika mchezo mwingine Benfica waliwafunga Anderletch 2-0 , Shakhtar Donetsk wakashinda ugenini dhidi ya Real Sociedad na Juventus na Fc Copenhagen walitoka sare ya 1-1 .
Matokeo ya mechi za Ligi ya mabingwa .
Manchester United 4-2 Bayer Leverkusen .
Galatasaray 1-6 Real Madrid.
Real Sociedad 0-2 Shakhtar Donetsk .
Fc Copenhagen 1-1 Juventus .
Olympiakos 1-4 Paris St Germain.
Benfica 2-0 Anderletch.
Viktoria Plzen 0-3 Manchester City
Bayern Munich 3-0 CSKA Moscow.
Michuano hiyo itaendelea hii leo ambapo Arsenal watakuwa wageni wa Olympique Marseile , Napoli watacheza na Borrusia Dortmund , Fc Barcelona watakipiga na Ajax Amsterdam , Ac Milan watacheza na Glasgow Celtic , Chelsea watakipiga na Fc Basel , Atletico Madrid watakuwa mzigoni na Zenith St Petersburg , Schalke wakicheza na Steua Bucharest huku Austria Wien wakicheza na Fc Porto.
Ratiba ya Mechi za Leo.
Chelsea vs Fc Basel .
Schalke vs Steua Bucharest.
Olympique Marseile vs Arsenal.
Napoli vs Borrusia Dortmund .
Atletico Madrid vs Zenith St Petersburg .
Fc Barcelona vs Ajax Amsterdam.
Ac Milan vs Glasgow Celtic.
Austria Wien vs Fc Porto
Story Za Michezo Kwa Hisani Ya Benki Ya NMB.