Quantcast
Channel: Millard Ayo
Viewing all articles
Browse latest Browse all 31461

Mourinho kampa Rooney saa ngapi?

$
0
0
Rooney amepewa saa 48 za kuamua kuondoka au kubaki United.

.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amempa mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney saa 48 za kufanya maamuzi, yakiwa ni maneno aliyoyatoa wakati anajibu maswali ya waandishi wa habari juu ya Rooney baada ya mchezo wa ligi ya England uliozikutanisha United na Chelsea Old Trafford na kushindwa kufungana August 26 2013.

Mourinho kasema Rooney ndie aliyeanzisha story za kutaka kuihama United kwa kumwambia mtu wake wa karibu kuwa yuko tayari kwenda Chelsea na ni wakati wake (Rooney) kumaliza story hiyo kwa kuamua kubaki au kuiambia United wazi kuwa anataka kuondoka.

Taarifa ikufikie kwamba Rooney alicheza mechi dhidi ya Chelsea kwa kiwango kikubwa na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo japo amekua kwenye kipindi kigumu akihusishwa na kuihama Manchester United mara kadhaa huku kocha wake David Moyes akisisitiza BIG NO, yani hauzwi mtu.

Mourinho amesema kuwa anampa Roney saa 48 za kufanya maamuzi ambapo kama ataamua kubaki United basi wataheshimu uamuzi wake na wataachana naye na kutafuta suluhu ya kusajili mshambuliaji mwingine ambapo kwenye headlines nyingine, stori zilizotoka August 26 2013 ziliamplfy kwamba wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o amewasili London tayari kuanza mazungumzo na watu wa Chelsea.

Story Za Michezo Kwa Hisani Ya Benki Ya NMB.

Use Facebook to Comment on this Post


Viewing all articles
Browse latest Browse all 31461

Trending Articles