Chid Benz baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kesho August 13 2013 anategemea kutoa single mpya ambayo yeye mwenyewe hajaipa jina hadi hivi sasa….. karekodi hii single baada ya kutoka Kenya alikofanya kazi pamoja na Nonini.
Mkali kutoka La Familia bado anasema baada ya kukaa kimya kirefu na mashabiki wake kum-miss sana, anakuja na kitu ambacho watamjua Chid Benz yule wa Dar es salaam stand up.
“Nimerekodi ngoma na Ommy Dimpoz lakini watu wangu wa karibu wamenishauri kutoa ngoma hii ambayo nimefanya kwa Ema the boy na ndani yake nipo peke yangu, kesho watu wangu watapata nafasi ya ku-download hapahapa”.