Quantcast
Channel: Millard Ayo
Viewing all 31461 articles
Browse latest View live

Christian Bella ametuletea hii video mpya, ‘Yanga kiboko yao’

$
0
0

Ni Mkali Christian Bella ambae time hii ametuletea video mpya ya single yake iitwayo Yanga Kiboko yao.

 


Picha: Wachezaji wa Yanga SC wakifanya mazoezi kujiandaa na msimu mpya 2023/24

$
0
0

Ni Wachezaji wa Young Africans ambao wapo kambini wakijiandaa ama wakifanya mazoezi yao ya kila siku kwaajili ya kujiweka sawa katika msimu mpya wa 2023/24.

Hapa nimekusogezea picha kadhaa ushuhudie kile kinachoendelea Kambini.

.

.
.
.
.
.
.
.
.

Aidha Yanga SC wanatarajia kufanya shamra shamra ya Wiki ya Mwananchi Julai 22, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Picha: Kramo, Che Malone, Onana na Baleke waanza mazoezi kambini Uturuki

$
0
0

Ni Wachezaji wa Simba Sports Club ambao wameweka kambini nchini Uturuki kwaajili ya kujiandaa na michuano ya msimu wa 2023/24 utakaoanza hivi karibuni.

Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji wakifanya mazoezi  ya kuimarisha miili yao. wakiwemo Kramo, Che Malone, Onana na Baleke.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Good news kutoka GSM zikufikie popote ulipo, leo nakutembeza Home BOX ushuhudie bidhaa mpya

$
0
0
Good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba GSM wanatangaza uzinduzi wa Asante Card zenye mchakato wa kukupatia zawadi za papo hapo.

Ukiwa na Asante Card utapata nafasi ya kupata punguzo la asilimia 5%  kila unapofanya manunuzi ya katika madukan ya GSM ikiwemo Splash, Babyshop, Max, Shoexpress, GSMsports.

Na pia kila Mwanachama wa Asante Card anauwezo kupokea taarifa maalumu kuhusiana na  Mauzo pamoja na matukio maalumu kabla taarifa hiyo haijafika kwa umma.

Jiandikishe sasa na Asante Card kwenye maduka ya GSM ufurahie huduma zao na punguzo hilo la kibabe.

Na leo Julai 19, 2023 millardayo.com imetembelea Home Box iliyopo Msasani Mall tazama bidhaa mpya za kibabe.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Dereva Halima aliyekatika Mkono apata Mkono wa Umeme, aanda tuzo kwa Rais Samia (video+)

$
0
0

Ni Halima Mbwana ambae aliwahi kuingia katika vichwa vya  habari baada ya kupata ajali katika basi alilokuwa akiliendesha la kampuni ya Super Feo kisha kupelekea kukatika Mkono wake.

Sasa leo Julai 19, 2023 ameimbia Millardayo.com & Ayo TV  namna Serikali ilivyomsaidia ama kufanikisha kupata Mkono bandia wa Umeme ambao utamsaidia katika shughuli zake.

Rais Samia aupeleka mradi wa Uboreshaj Usalama wa Milki za Ardhi Mbinga ‘Migogoro itaisha’

$
0
0

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiwezesha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuupeleka mradi wa Uboreshaji wa Miliki salama za Ardhi kwa maeneo ya Vijijini katika Halmashauri saba hapa nchini ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ni miongoni mwake.

Mradi huo una lengo la kumaliza migogoro ya matumizi ya ardhi na migogoro ya mipaka ya vijiji na kutumika kama dira ya matumizi sahihi ya kila kipande cha ardhi ndani ya Halmashauri huku ukitoa njia sahihi za kusimamia utunzaji wa maeneo ya hifadhi za vilele vya milima, misitu na vyanzo vya maji.

Akiongea leo wakati wa kikao cha Wadau kujadili rasimu ya Mpano huo, katika Halmashauri ya Mbinga, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga, Pendo Ndumbaro ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo  amesema Mpango huu itapendeza ukiweka maeneo ya kimkakati ya uwekezaji kutokana na rasilimali zilizopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Mbinga.

Tuna kila sababu ya kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kunufaika na Mradi huu, moja ya vipengele muhimu wakati wa utekelezaji wa mradi huu ni Kuandaa Mpango wa Matumizi ya ardhi ya Halmashauri ya wilaya ambao umekwisha andaliwa Rasimu na sasa ni zamu yetu kama wadau muhimu wa maendeleo ya Halmasahuri ya wilaya ya Mbinga kupitia mpango huu na kutoa maoni yetu”

Mpango huu ni wa miaka ishirini (20) ijayo kuanzia mwaka huu 2023 mpaka 2043 ukiwa na Lengo kuu la kusimamia matumizi ya ardhi na kuimarisha ukuaji wa uchumi wa watu wanaoishi katika Halmashauri ya wilaya kwa kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali ardhi na kuzingatia uhifadhi wa mazingira.

.Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo akizungumza katika Mkutano huo

 

 

Hatimae Yanga washusha kifaa kutoka Afrika Kusini Skudu mtu fundi kutoka Malumo

$
0
0

Yanga SC wamemtambulisha rasmi atakayevaa jezi namba 6 ambaye ni Mahlatse Makudubela (Skudu) Raia wa Afrika Kusini, amejiunga na Yanga kama Mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

Skudu amewahi kucheza Timu mbalimbali zikiwemo Mamelod Sundowns, Orlando Pirates, Highland Park na Chippa United zote za Afrika Kusini.

Yanga SC yamsajili Skudu, Utambulisho wake kipekee, Jux amfundisha kuicheza style hii

$
0
0

Yanga SC wamemtambulisha rasmi atakayevaa jezi namba 6 ambaye ni Mahlatse Makudubela (Skudu) Raia wa Afrika Kusini, amejiunga na Yanga kama Mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

Skudu amewahi kucheza Timu mbalimbali zikiwemo Mamelod Sundowns, Orlando Pirates, Highland Park na Chippa United zote za Afrika Kusini.

Sasa Uongozi wa Young Africans wameamua kumtumia Juma Jux na wimbo wake kwenye kunogesha shangwe za kumkaribisha Skudu, unaweza ukaonyeza play ushuhudie Skudi akicheza wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux.


Video: Dulla Makabila na Sholo Mwamba wajipanga kuwaburudisha Wana Yanga ‘Wiki ya Mwananchi’

$
0
0

Ikiwa zimebaki siku chache Kuelekea Wiki ya Mwananchi ya Young Africans inayotarajiwa kufanyika Julai 22,2023 pale katika uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam.

Hapa tumekusogezea Miongoni mwa wasanii ambapo wameshatangazwa kutoa burudani siku hiyo ni ambao ni Dullah Makabila, Sholo Mwamba, Mavokali

 

Tambo za Sholo Mwamba kuelekea siku ya Wiki ya Mwananchi Julai 22,2023 Burudani Mwanzo mwisho

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo July 19, 2023

$
0
0

Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam July 19, 2023,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.

Habari kubwa Magazetini Kenya leo July 19, 2023

$
0
0

Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania July 19. 2023,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini kenya.

Singapore namba moja Passport Duniani yaipiku Japan

$
0
0

Nchi ya Singapore imeiondoa Japan kwenye namba 1 ya orodha ya Nchi zinazomiliki passport zenye nguvu duniani baada ya Nchi hiyo kufikisha Nchi 193 ambazo Raia wake wanao uhuru wa kuingia bila kutakiwa kutuma maombi ya VISA kabla.

Wakati Singapore ikifikisha Nchi hizo 193 kati ya 227, nafasi ya pili nayo imechukuliwa na Ujerumani, Italia na Hispania ambazo zote kwa pamoja passport zao zimeongezewa nguvu kutokana na kufikisha Nchi 190.

Japan imeporomoshwa hadi nafasi ya tatu ambako imefungana na Korea Kusini, Austria, Finland, Ufaransa, Luxembourg na Uswizi ambapo Raia kutoka Nchi hizi 7 watafurahia uhuru wa kusafiri kwa kuingia Nchi 189 muda wowote wanaotaka bila kufata mlolongo mrefu ambao ingewalazimu kusubiri siku kadhaa kupata ruhusa ya VISA kabla ya kusafiri.

Mataifa maarufu duniani kama Marekani na Uingereza mara yao ya mwisho kushika nafasi ya juu kwenye chati hizi ilikua ni mwaka 2014 ambapo zote kwa pamoja zilifungana kwa kushika nafasi ya kwanza lakini kwa mwaka huu Marekani imeshika namba 8 ikiwezesha Raia wake kuingia Nchi 183 huku Uingereza ikishika namba 4.

Singapore ambayo hadi 2021 ilikua na Watu milioni 5.4 ilipata uhuru wake kutoka kwa Malaysia August 9 mwaka 1965.

Big Joe kaleta Mchongo, buku yako inaweza ikatimiza ndoto yako, wahi sasa

$
0
0

Lengo la Big Joe ni kuhakikisha kila Mwenye ndoto anatimiza , hakuna vigezo wala masharti hii ni kiingilio tu , tenga BUKU sikiliza XXL mwisho wa kipindi upate LAKI SITA .

Zawadi za MchongoPesa zinatolewa kila siku kwenye Vipindi mbalimbali vya #cloudsfm , inakuhitaji kuwa na BUKU tu .!! Ila Kujishindia hadi Mamilioni na zawadi Kibao

Hatua za kushinda zawadi hiyo na nyinginezo ni 👇

HATUA 1. Bonyeza menu yako ya malipo

HATUA 2. Chagua Lipia Bili.

HATUA 3. Kisha weka namba ya Kampuni (321333).

HATUA 4: Ingiza namba ya kumbukumbu (Andika neno PESA).

HATUA 5: Weka kiasi 1000.

HATUA 6: Ingiza namba yako ya SIRI.

HATUA 7: Bonyeza 1 KUTHIBITISHA AU 2 KUKATAA.

Ushiriki ni Miaka 18 na Zaidi, Masharti na Vigezo Kuzingatiwa.

Jezi 5 mpya za Namungo zilivyozinduliwa na Waziri Mkuu Majaliwa

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa July 18, 2023 ameshuhudia uzinduzi wa jezi ya Timu ya mpira wa miguu ya Namungo ya msimu wa 2023/2024 ambapo hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Kassim Majaliwa, Ruangwa, Lindi.

 

Mabibi na Mabwana Young Dee na Ally B wametuletea hii single mpya ‘Basupa’ isikilize hapa

$
0
0

Ni muda mwingine tena wa Rapper Young Dee ( @youngdaresalama ) kupita na maokoto yake baada ya ukimya wa zaidi ya mwaka mmoja bila kuachia goma lolote lakini sasa amewa-bless Raia na kitu kipya kinaitwa ‘basupa’ ft. @djallybi kinachopatikana kwa audio kwenye platform mbalimbali.

Flow zake, uandishi wake na level yake ya kupita juu ya mdundo wowote ndio vimemfanya kuendelea kuishi kwenye playlist zetu hata kama hana goma jipya na sasa leo ni siku rasmi ya kuanza kutetema na hili dude lake jipya la ‘basupa’ ambalo video yake inatoka wiki ijayo.

Jina lake lilianza kuhesabiwa kwenye Top 10 za fleva za Bongo na kuanza ku-shine toka mwaka 2009 alipomaliza kidato cha nne na kuachia ngoma yake ya ‘Teacher’ japo ngoma yake ya kwanza kuitoa ilikua ‘tafsiri’ ambayo aliiachia mwaka 2007 akiwa bado Mwanafunzi.

Kuanzia sasa na kuendelea nitakua nakuwekea ngoma mpya za Wakali wa Bongo mida ya asubuhi ili uishibishe playlist yako na pini mpya.……. kama kwa kipisi hiki tu umekubali jinsi Young D alivyopita na huo mdundo dondosha emoji yoyote nzito iliyokaribu nawe


Kassim Mganga kaileta hii video mpya ya wimbo wake uitwao ‘Jero’, unaweza ukabonyeza kuitazama

$
0
0

NI Mkali kutokea Bongo Flevani, Kassim Mganga ambae time hii ametuletea hii video mpya ya single yake iitwayo Jero.

Unaweza ukabonyeza play kuitazama kisha usisahau kuandika neno lolote ili mkali huyo akipita asome mlichomuandikia.

“Wewe unaongea hovyo, unamtukana Mama, Rais, umekosea tutakuadhibu” Nape amvaa Lissu

$
0
0

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknoloji ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amewataka watanzania kutotumia lugha za matusi kukosoa jitihada mbalimbali zinazofanywa chini na Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Julai 18 Mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza Katika Kongamano la Majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi.

Serikali imekamilisha mradi wa maji katika kijiji cha Migongo mkoani Kigoma, Aweso azungumza haya

$
0
0

Serikali imekamilisha mradi wa maji katika Kijiji cha Migongo Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma na kuwaondolea wananchi adha kubwa ya upatikanaji wa huduma hiyo waliyokuwa wakikabili tangu kupata uhuru.

Mradi huo wenye thamani ya shiling bilioni 1.1  hadi sasa umefikia asilimia 98 na kuzinduliwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambapo wananchi Elfu kumi na nne wameanza kufaidika na upatikanaji wa maji safi na salama.

Mwaka 2022 matumaini mapya ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Kijiji cha Migongo yalianza baada ya utekelezaji wa mradi wa maji kuanza na sasa Waziri Jumaa Aweso ameuzindua.

Kwa miaka yote walilazimika kutembea umbali mrefu na hata kupanda milima kutafuta huduma hiyo muhimu lakini bado kiu yao ilikuwa ni kuona mradi wa maji unafika katika eneo lao.

Baada ya uzinduzi wa mradi katika Mkutano na wananchi Waziri wa Maji Jumaa Aweso anatoa angalizo kwa kamati ya mradi huo ,kukusanya ankara za maji na kutumia fedha hizo kuendeleza mradi na sio matumizi binafsi.

Katika wilaya ya kasulu Mradi wa maji unaogharimu shilingi bilioni 1.2 kwa ufadhili wa shirika la Water Mission nao umezinduliwa na kutarajiwa kunufaisha karibu wakazi elfu 62 wa Vijiji vitatu vya kata ya Makere ambao walikuwa wakikabiliwa na adha hiyo.

.
.
.
.
.
.
.
.

GSM Home wamekuletea hizi bidhaa za ndani leo Julai 19, 2023, wahi sasa inogeshe nyumba yako

$
0
0
Ni Wakali wa bidhaa za ndani hawa si wengine niGSM Home ambapo wanakukaribisha wewe mtanzania ufike kwenye maduka yao kujionea  muonekano mpya wa vitu vya nyumba.

Ikiwa leo ni Jumatatu tulivu basi fika GSM HOME iliyopo Mikocheni, Mlimani City, Masaki ( Haile Sellasie), Salamander Tower ( Samora Avenue) na Dodoma ‘Capital City Mall) ama wapigie namba 0745 000 000 karibu wakuhudumie, karibu uinogeshe nyumba yako.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Mstaafu Kikwete ahojiwa Power Breakfast, ajibu matumizi ya mtandao wa internet wakati akiwa Rais

$
0
0

Radio show ya asubuhi ya Power Breakfast @CloudsFMTZ leo July 19 2023 imefanya mahojiano na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Arusha na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo nafasi yake kwenye matumizi ya mtandao wa Internet wakati akiwa Rais.

Mstaafu Kikwete alisema kwenye utawala wake mwaka 2005 hadi 2015 vita dhidi ya rushwa alipambana nayo sio tu kwa Watuhumiwa kupelekwa Mahakamani lakini pia aliwekeza kwenye mkongo wa Taifa uliosambaza mtandao wa internet kwa kiwango kikubwa ili kuuondoa utaratibu wa kulazimisha Wananchi kufata huduma za kiserikali dirishani na badala yake kutumia mtandao ili kupunguza mianya ya rushwa kati ya Mtoa huduma na mpewa huduma.

Alipoulizwa kuhusu misemo yake maarufu ikiwemo ‘akili za kuambiwa changanya na zako’, Mstaafu Kikwete alijibu kama ifuatavyo “Ujumbe wangu pale ni kwamba unapopewa nafasi ya uongozi usiwe unafanya yale unayoambiwa tu, utasikia mengi lakini baada ya pale tafakari uweze kuchambua chuya na mchele, kwenye nafasi ya uongozi tatizo lake ni kwamba kama sio muangalifu utaumiza Watu”

Kipindi hiki maarufu cha asubuhi ambacho husikika kuanzia saa kumi na moja alfajiri hadi saa nne asubuhi kimefanya mahojiano haya Jijini Arusha ambako kunaendelea Mkutano unaojadili demokrasia Barani Afrika uliohudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu Kikwete.

Fanya kupita kwenye Youtube ya CLOUDS MEDIA ili utazame Interview hii kubwa ya siku iliyofanywa na Wakali wa hizi kazi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by millardayo (@millardayo)

Viewing all 31461 articles
Browse latest View live